Adbox

Tuesday, November 26, 2019

Rushwa ya ngono kazini yakemewa

Jukwaa la wanawake mkoani Kilimanjaro limekemea vikali vitendo vya rushwa ya ngono katika taasisi binafsi na Umma na kuunga mkono juhudu zilizofanywa na Serikali katika kukabiliana na tatizo hilo ambalo linadaiwa kukandamiza haki na usawa kwa wanawake katika jamii.

Jukwaa hilo linajumuisha wanawake kutoka wilaya sita za mkoa huo ambao wamesema aina hiyo ya ruhwa imekuwa kikwazo katika maeneo ya kazi na kusababisha utendaji kazi kwa waarhirika kushuka kiwango sanjari na kuzusha hofu.

Wamesema vitendo hivyo vimekithiri zaidi katika sekta mbalimbali zikiwemo sekta za elimu, afya na ajira na hivyo kuongeza maambukizi ya UKIMWI licha ya Serikali kufanya jitihada nyingi kuhakikisha inatokomeza maambukizi mapya na kukomesha vitendo hivyo.

Akizungumza katika jukwaa hilo, Mwenyekiti wa Bodi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Asseny Muro amesema, rushwa ya ngono katika maeneo ya kazi imekuwa ikishika kasi kutokana na baadhi ya viongozi wenye mamlaka kuendekeza vitendo hivyo kwa maslahi binafsi huku wakitumia mwanya huo kuwanyima fursa ya kupata ajira watumishi wenye weledi na utendaji wa ufanisi.

No comments:

Post a Comment

Adbox