Adbox

Wednesday, November 20, 2019

Rais Magufuli atoa neno kupanda kwa bei ya mahindi

Rais John Magufuli ameongea na Wakazi wa Morogoro leo na kusisitiza kuwa katika kipindi chake cha uongozi hatopanga bei ya mkulima kuuza mazao yake.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo akiongea na wananchi wa Msamvu, Morogoro akiwa njiani akielekea mkoani Dodoma.

"Ukiona wengine wachache wanalalamika bei ya mahindi iko juu, najua wakulima wanashangilia, na nataka wakulima washangilie zaidi,tulizungumze hili wazi kwa watanzania wote, ukiona mahindi yako juu nenda kalime yako ya bei ya chini biashara hii lazima iwe huru" amesema Rais Magufuli.

Katika hatua nyingine Rais Magufuli amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa NIDA kufika Mkoani Morogoro leo na ikiwezekana akae Mkoani humo hata siku tatu ili kushughulikia tatizo la Watu wengi kukosa vitambulisho vya Taifa huku Mkoa mzima ukiwa na Ofisi moja pekee ya NIDA.

No comments:

Post a Comment

Adbox