Adbox

Wednesday, November 20, 2019

Ridhiwani Kikwete aipongeza serikali kwenye hili

Mbunge wa Jimbo la Chalinze wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, Ridhiwani Kikwete ameipongeza serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli kwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa wananchi kwa wakati.

Kiongozi huyo ametoa pongezi hizo kijijini Mwidu kata ya ubena wakati wa zoezi la uwashaji wa umeme.

Alisema kuwa Rais Magufuli amekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha miradi yote iliyoahidiwa kwa wananchi inatèkelezeka.

"Nimekuwa nikifarijika sana kuona miradi mikubwa yenye tija ikifanikiwa kuwepo katika jimbo langu"Alisema Kikwete.

Aidha mbunge huyo amewataka wananchi wa Ubena kutumia fursa ya kuwashwa kwa umeme kwa kuanzisha biashara pia kuanzisha viwanda vidogovidogo ili kuweza kujiongezea kipato.

Naye Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu amewahakikishia wananchi wa jimbo la Chalinze kuwa serikali itaendelea kutekeleza ahadi zake kama ilivyoahidi kwa wananchi wake.

Aidha alisema kuwa serikali imelipia nguzo zote hivyo hakuna mwananchi kutozwa bei ya kununua nguzo bali cha msingi ni kulip

No comments:

Post a Comment

Adbox