Mkutano maalum wa tano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa kauli moja umekubali na kuridhia ongezeko la mtaji wa Benki hiyo kutoka dola za kimarekani bilioni 90 hadi dola za kimarekani 283 kutokana na uwepo wa majadiliano juu ya kiwango cha ongezeko la mtaji wa Benki hiyo.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo maalum wa tano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) uliofanyika Abidjan Nchini Ivory Coast na kuhudhuriwa na Rais wa Nchi hiyo Mhe. Alassane Ouattara, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi amesema maamuzi yaliyopitishwa na magavana wa Benki hiyo waliohudhuria mkutano huo ni ya kihistoria ambapo sasa inaifanya Benki ya Maendeleo ya Afrika kushika nafasi ya pili duniani baada ya Benki ya Dunia.
Amesema kuwa uamuzi huo unaifanya Benki ya Maendeleo Afrika kuwa na uwezo mkubwa wa kufadhili na kuhisani miradi mbalimbali na mikubwa ya kimkakati katika Bara la Afrika Tanzania ikiwemo na hivyo kuliwezesha bara hilo kupiga hatua kubwa za kimaendeleo
Prof. Kabudi amezitaja faida ambazo nchi za Afrika itazipata kutokana na kuongezeka kwa mtaji wa Benki hiyo ikiwa ni pamoja na kuwa na uwezo wa kutoa mikopo mikubwa na ufadhili kwa ajili ya kutekeleza miradi mikubwa nay a kimkakati kwa ajili ya kuliendeleza bara hilo husani katika miundo mbinu,nishati na hudumu muhimu za kijamii ambayo nchi nyingi za kiafrika ambazo ni wanachama wa Benki hiyo walishindwa kuitekeleza kutokana na ukosefu wa rasilimali fedha.
Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Dkt. Yamungu Kayandabila kwa upande wake amesema kutokana na Bara la Afrika kuwa na Nchi nyingi masikini uwepo wa Benki ya Maendeleo ya Afrika inatoa ahueni kwa Nchi hizo na kutoa wito pia kwa taasisi binafsi kutoka Nchi za Kiafrika kuchangamkia fursa ya ongezeko la mtaji wa Benki hiyo kutokana na ukweli kuwa AfDB inakopesha pia taasisi binafsi.
Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) ambayo illianzishwa kwa lengo la kuchochea maendeleo ya Bara hilo ikiwa na jukumu la kutafuta rasilimali fedha kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya kimkakati kwa maendeleo ya kiuchumi ya Afrika inamilikiwa kwa asilimia 60 na Nchi za Kiafrika na asilimia nyingine 40 zilizosalia zinamilikiwa na nchi waalikwa kutoka katika mabara mengine duniani Marekani ikiwemo.
Saturday, November 2, 2019
Mkutano maalum waridhia ongezeko la mtaji wa AfDB
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment