Adbox

Tuesday, November 26, 2019

Bilioni 124 zilizopotea vyama vya ushirka, ripoti yakabidhiwa kwa TAKUKURU

Ripoti ya shirikisho la ukaguzi wa vyama vya ushirika labaini Vyama vya ushirika asilimia 94 vina viashiria vya ubadhilifu wa zaidi ya Bilion 124.53 baada ya vyama hivyo kupata hati zisizoridhisha, hati zenye mashaka na hati chafu.

Akikabidhi Ripoti hiyo kwa Naibu mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Waziri wa kilimo Japheti Hasunga amesema kuwa kati ya vyama 4413 vilivyokaguliwa vyama 303 ndivyo vilivyopata hati safi ikiwa ni sawa na asilimia 6.

Pia amesema ripoti hiyo imebaini uwepo wa waajiri wasiofikisha michango ya wafanyakazi wao katika Vyama vya kuweka na kukopa wakiwemo wakurugenzi wa halmashauri mbalimbali na Taasisi za serikali.

No comments:

Post a Comment

Adbox