Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimetiliana saini makubaliano ya mashirikiano na Baraza la Biashara la Uholanzi-Afrika (NABC) hapo jana Novemba 25, 2019 katika Ofisi za TIC, Dar es Salaam.
Makubaliano hayo yamesainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Geoffrey Mwambe na Mkurugenzi Mkuu wa NABC Bw. Peter Ruiter na yamelenga kujenga mfumo wa pamoja wa kufanikisha biashara na uwekezaji zaidi baina ya Tanzania na Uholanzi.
Maafikiano ya makubaliano hayo ni matokeo ya mkutano uliofanyika kati ya TIC na NABC nchini Uholanzi, Februari, 2019.
NABC ina makampuni wanachama zaidi ya 300 ambayo yamewekeza katika sekta mbalimbali nchini Uholanzi na Sekta hizo ni pamoja na kilimo na kuongeza thamani, viwanda (nguo, maziwa), afya nishati, bandari, ujenzi, mifugo na kuongeza thamani.
Tuesday, November 26, 2019
Baraza la Biashara la Uholanzi-Afrika kunadi fursa za Uwekezaji
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment