Adbox

Saturday, October 19, 2019

Waziri Mahiga atolea ufafanuzi tuhuma za Kompyuta za DPP kuibwa

Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Balozi Agustine Mahiga ameweka bayana kuwa vipande vya kompyuta vilivyoibiwa ni vya ofisi ya Mashtaka Mkoa wa Dar es Salaam na siyo ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) nchini Tanzania.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Balozi Mahiga pia akawataka watu kuliachia jeshi la polisi liendelee na uchunguzi wake unaofanywa kupitia vipande vya komputer vilivyobaki.

“Hakuna athari zozote za kiutendaji katika ofisi hiyo na wanaendelea na kazi yao kama kawaida,” Waziri Mahiga.

Ameendelea kwa kusema, "Ofisi ambayo ilivunjwa na vipande vya Kompyuta kuchukuliwa ni ya Mkoa wa Dar es Salaam, Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu anayeshugulikia mashitaka ya Serikali haikuguswa, nyaraka zote zipo, taarifa zote zipo na kazi zake zinaendelea".

No comments:

Post a Comment

Adbox