Adbox

Saturday, October 19, 2019

Ndege nyingine aina ya Bombardier Q400 kutua nchini, serikali yasaini mkataba

Serikali ya Tanzania imesaini mkataba na kampuni ya kutengeneza ndege kutoka Canada kwa ajili ya ununuzi wa ndege mpya aina ya Bombardier Q400, inayotarajiwa kufika nchini June 2020, yenye kubeba abiria 78 na uwezo wa kutua katika viwanja karibia vyote nchini.

Mkataba huo umesainiwa leo ambapo Mkurugenzi wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) Ladislaus Matindi, amesema kuwa ujio wa ndege hiyo unalengo la kuhakikisha inakuza huduma za usafiri wa ndege hapa nchini.

''Tunanunua ndege kulingana na mpango wetu wa biashara na kwa hali ya soko la sasa hivi hizo ndege 11 na hizo ndege zingine zilizokuwa zimetumika zinatupa sisi uwezo wa kutoa huduma kutokana na matakwa ya soko, lakini soko linabadilika na kwa makisio yetu hadi 2022 hizi ndege zitatufikisha hapo bila matatizo yoyote'' amesema Matindi.

Aidha matindi ameongeza kuwa hadi sasa ATCL wana jumla ya ndege 6, ambapo hadi mwisho wa mwaka huu kutakuwa na jumla ya ndege 8 na kwamba hadi kufikia mwaka 2021, Shirika hilo litakuwa na jumla ya ndege mpya 11.

No comments:

Post a Comment

Adbox