Adbox

Saturday, October 19, 2019

Katibu Mkuu Wizara ya Afya atembelea Hospitali ya Rufaa ya Bugando

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dkt. Zainab Chaula ametembelea Hospitali ya Rufaa ya Sekou Toure kukagua ujenzi wa jengo la ghorofa litakalotoa huduma mbalimbali kisha kutembelea baadhi ya maeneo ya utoaji wa huduma za afya, kuongea na wagonjwa waliofika Hospitalini hapo ili kupata huduma lengo likiwa ni kusikiliza kero zao na kuzitafutia ufumbuzi kisha amehitisha kwa kuongea na watumishi na kutatua baadhi ya kero alizoziona.

Baada ya hapo Dkt. Chaula ametembelea Hospitali ya Rufaa ya Bugando na kuzungumza na Menejimenti ya Hospitali hiyo na kuridhishwa na mafanikio yaliyopatikana ndani ya kipindi cha miaka miwili na kuwezesha hospitali kutoa huduma bora na kuongezeka kwa ukusanyaji wa mapato.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Bugando Prof. Abel Makubi amepongezwa kutokana na ubunifu wake uliowezesha hospitali kuboresha miundombinu na mapato ya ndani.

Dkt. Chaula pamoja na timu aliyoambatana nayo akiwemo Mkurugenzi wa Tiba Dkt. Grace Maghembe imeishauri Hospitali ya Bugando kuendelea kuzijengea hospitali za Mikoa na Wilaya katika kuzalisha maji tiba kwa wagonjwa. Asilimia 50 ya infusion zinazotumika Bugando zinazalishwa na hospitali.

Prof. Kabudi ameishukuru serikali kupitia wizara ya afya  kwa kusaidia kuanzishwa huduma za wagonjwa wa saratani kupitia ujenzi wa jengo la huduma hizo. Pia aliendelea kushukuru kwa hospitali hiyo kuingizwa kwenye mpango wa kupata  mashine ya MRI.

Dkt. Chaula na timu nzima anayoongozana nayo imeondoka jijini Mwanza kuelekea Chato na Geita kuendelea na ziara yake katika mikoa ya kanda ya ziwa.

No comments:

Post a Comment

Adbox