Adbox

Tuesday, October 22, 2019

UDSM kutoa mitihani ya Kiswahili Kimataifa

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk. Leonard Akwilapo amesema kuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kinatarajia kuanza kutoa Mitihani ya Kimataifa ya Ujuzi wa Lugha ya Kiswahili (MKUKi) kuanzia Januari mwakan 2020.

Hayo ameyasema leo jijni Dodoma wakati akitoa taarifa hiyo ya mitihani kwa waandishi wa habari waliohudhuria Mkutano huo.

Dk. Akwilapo amesema kuwa  hatua hiyo ni jitihada za kuikuza na kuieneza Lugha ya Kiswahili ulimwenguni kwa kuwa ni miongoni mwa lugha 10 zenye wazungumzaji wengi duniani.

” Lengo letu ni kuunga mkono juhudi za Serikali za kukieneza Kiswahili na kusimamia ubora wake ambapo sasa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kimechukua jukumu la kuanzisha mitihani ya Kimataifa ya Ujuzi wa Lugha ya Kiswahili sanifu ili lugha ya kimataifa ipate nguvu zaidi hutungiwa mitihani ili wanaojifunza lugha hizo waweze kutathminiwa na kupata vyeti,” Amesema Dk Akwilapo.

Dk.Akwilapo amesema kuwa mitihani itafanyika mara sita kwa mwaka ikiendana na kipindi cha masomo ya Kiswahili kwa kila ngazi na itafanyika kwa njia za kielektroniki katika vyuo na vituo mbalimbali vya Kiswahili duniani.

“CKD(Udsm), kinakuwa ni Chuo Kikuu cha kwanza duniani kutunga mitihani hii na kusimamia utahini na usahihishaji wake na kutoa Cheti cha Kimataifa kinachoonesha kiwango cha ujuzi wa mtahiniwa,”amesema Dk.Akwilapo

Hivyo Chuo kinabeba  jukumu la kuanzisha mitihani ya Kimataifa ya Ujuzi wa Lugha ya Kiswahili sanifu na ili lugha ya kimataifa ipate nguvu zaidi hutungiwa mitihani ili wanaojifunza lugha hizo waweze kutathminiwa na kupata vyeti.

Ameeleza kuwa tayari kuna makubaliano baina ya walimu wa Kiswahili wa CKD na walimu wanaofundisha Kiswahili katika vyuo vya nje kuhusiana na mitihani hiyo ambayo itaanza kutolewa mwakani.

“CKD imejiandaa kuhakikisha kuwa mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano iko madhubuti kuwezesha mitihani hii kufanyika kwa ufanisi na kwa viwango vya kimataifa kwani kuna wahitaji ambao watafanyia mitihani hii wakiwa katika nchi zao, sio lzima wasafiri na kuja kufanyia mitihani yao hao Tanzania,”aliongeza

Aidha amefafanua kuwa walengwa wa mitihani hiyo ni watu wote ambao wanajifunza Kiswahili kama lugha ya pili au lugha ngeni katika ngazi mbalimbali ikilenga kupima usanifu katika kusoma, kuandika, kuongea na kusiukichangia ambapo amesema wanaamini wanapaswa kuongeza juhudi za kukuza Kiswahili ili kumuenzi Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye alifanya jitihada kubwa za kueneza na kukuza lugha hiyo katika Nchi za Afrika na duniani kwa ujumla.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Taaluma za Kiswahili, Prof.Aldin Kai Mutembei, amesema kuwa mitihani hiyo itaitwa kwa jina la MKUKi.

Prof.Mutembei amesema kuwa kuna wanafunzi  wanasoma Kiswahili huko nje na walitamani kuja kwenye nchi zinazozungumza Kiswahili lakini wangependa wawe na utambulisho kuwa wanajua Kiswahili hawa ndio tunaowalenga.

No comments:

Post a Comment

Adbox