Adbox

Tuesday, October 22, 2019

TFF yafanya mabadiliko mechi ya Simba SC na Azam FC

Bodi ya Ligi kupitia Shirikisho la Soka Tanzania (TPLB) imefanya mabadiliko mchache kuelekea mechi ya Simba dhidi ya Azam Jumatano ya kesho.

Awali mechi ilipangwa kuchezwa saa 10 kamili katika Uwanja wa Taifa lakini baadaye ikapanguliwa na sasa itachezwa majira ya saa 11 za jioni.

Uamuzi wa kubadili muda wa mechi hiyo umekuja ili kuwapa nafasi mashabiki watakokuwa makazini kupata muda wa kuitazama mechi hiyo.

Mabadiliko mengine ni juu ya Uwanja ambapo awali ilipaswa mechi ichezewe Uhuru lakini kupitia Waziri mwenye dhamana ya michezo, Harrison Mwakyembe aliruhusu ipigwe kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Adbox