Adbox

Wednesday, October 30, 2019

TANESCO yakutana na wateja wakubwa wa umeme kanda ya kati

Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) limefanya mkutano na wateja wake wakubwa na wenye viwanda katika Kanda ya kati ambapo Kikao hicho kilihusisha wawekezaji wenye Viwanda katika Mikoa ya Morogoro, Dodoma na Singida.

Akifungua mkutano huo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma , Dkt Binilith Mahenge, amesema Serikali iliahidi kuwapatia watanzania huduma ya umeme iliyo bora na yenye uhakika ili kuweza kuwakwamua kiuchumi wananchi hisusan walioko maeneo ya vijijini, Ahadi hii inatekelezwa na Serikali kupitia TANESCO kwa kuwekeza katika Miradi mikubwa ya uboreshaji wa miundombinu ya umeme.

Kwa upande wake Meneja Mwandamizi TANESCO Kanda ya Kati Mhandisi Athanaius Nangali ambaye alimuwakilisha mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO katika kikao kazi hicho alisema kuwa TANESCO ina miradi mingi inayo endelea katika maeneo mbali mbali ya Kanda ya kati, akiitaja Miradi hiyo ni pamoja na ule wa Upanuzi wa Kituo cha kupoza umeme cha Singida kutoka Megawat 32 hadi kufikia uwezo wa Megawati 400 hii pia itawezesha watumiaji wa umeme wa Mkoa wa Singida na maeneo ya Jirani kuwa na umeme wa uhakika.

No comments:

Post a Comment

Adbox