Ligi kuu ya England wana mpango wa kuleta teknolojia mpya ya kuimarisha VAR ili kusaidia kuongeza usahihi na kasi ya maamuzi ya mipira ya kuotea.
Imeelezwa kuwa, teknolojia hiyo itakuwa inafuatilia na kunasa mguu wa nyuma wa kila mchezaji (kasoro kipa),huku ikiwa inatumia kamera nyingi ili kuwapa moja kwa moja waamuzi mstari wa Offside kwa ajili ya kutathimini papo hapo.
Teknlojia hii inakuja baada ya kuwepo na malalamiko mengi kuhusu kuchelewa kwa maamuzi ya VAR kwa njia ya sasa wanayoitumia kutambua makosa kama hayo ya Offside.
Matukio 26 yamepinduliwa na VAR katika mechi 100 za ligi kuu nchini England msimu huu, na teknolojia hiyo imeelezwa inakuja kwa ajili ya kuhusika na mipira ya kuotea tu.
Wednesday, October 30, 2019
Ligi Kuu ya England kuleta teknolojia ya kuimarisha VAR
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment