Adbox

Thursday, October 31, 2019

Tabora yaanza kutoza pesa kuingia stendi ya Mabasi yaendayo Mikoani

Na.  Rahel Nyabali,Tabora

Halmashauri ya manispaa ya Tabora imeanza kutoza fedha kama kiingilio cha kupata huduma ndani  ya stend Kuu ya mabasi mjini Tabora ikiwa ni chanzo kipya cha mapato na kuingiza  wastani  wa  shilingi  milioni  ishirini  kwa  mwezi  hili.


Kungia stendi ya mabasi mkoani humo ya pasa kutoa kiasi cha shilingi miambili ili kuingia ndani  kupata  huduma ya usafiri wa  mabasi yaendayo vijijini, wilayani na hata mikoani ambalo ni jambo jipya mkoani Tabora ukiringanisha na vituo vya mabasi  kwenye  baadhi mikoa mingine hapa nchini.

Masoud Sultan ni Mkazi  wa  Tabora mjini amesema  utaratibu wa kushangia kiasi hicho cha fedha  kutaweza kusaidia kuongeza mapato manispaa ya Tabora na kuletamaendeleo mkoani humo licha ya miundo mbinu katika stendi hiyo kutokwua rafiki.

Kaimu Mkurugenzi Halmashauri  ya Manispaa ya Tabora, Joseph Kashushula amesema hiki ni  chanzo kipya  cha mapato katika Halmashauri ya manispaa ya Tabora kwa lengo la kuongeza  mapato ya Serikali na kutumika kwa ajili ya maendeleo.

Aidha Mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa  ya Tabora, Joseph Kashushula amesema halmashauri itakuwa ikikusanya mapato zaidi ya shilingi  milioni 408 kwa  mwezi huku ikiendelea  na  mikakati ya kubuni vyanzo vingine vya mapato ya ndani.

No comments:

Post a Comment

Adbox