Adbox

Sunday, October 13, 2019

Shilingi milioni 150 zatengwa kwaajili ya mikopo kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu Kilwa

Na Ahmad Mmow, Kilwa Masoko.

Kiasi cha shilingi 150,000,000 milioni kimetengwa na halmashauri ya wilaya ya Kilwa kwa ajili ya mikopo kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.

Hayo yalisemwa jana kijijini Njinjo na msomaji wa taarifa ya mradi ya vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kwa kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa wa mwaka 2019, Mzee Mkongea Ali.

Msomaji taarifa huyo aliyesoma  kwaniaba ya mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kilwa, Renatus alisema ili kukamilisha asilimia 10 ya mapato ya ndani, shilingi 78,972,739.70 ziliingia katika mwaka wa fedha wa 2019\2020 ambazo tayari zimetolewa ka vikundi 23. Vikiwemo nane vya wanawake vilivyopatiwa mkopo wa shilingi 21,449095.60, vikundi 11 vya vijana vimepewa kiasi cha shilingi 30,649,096.30 na vikundi vinne vya watu wenye ulemavu vimepewa shilingi 26,874,547.80. Hivyo kuweza kukamilisha asilimia 100 ya lengo kulingana  na makusanyo ya mwaka wa fedha wa 2018\2019.

Alisema idadi ya vikundi vilivyopewa mikopo katika makundi yote ni 102 ambavyo vimekopeshwa
jumla ya shilingi 314,372,739.70 sawa na asilimia 100 ya makusanyo ya 2018\2019.

 '' Vikundi 50 vya wanawake vilikopeshwa shilingi 125,749,095.60, vikndi 43 vya vijana vilikopeshwa shilingi 125,749,096.30 na vikundi tisa vya watu wenye ulemavu vilikopeshwa kiasi cha shilingi 62,874,547.80,'' alisema.

Alisema halmashauri hiyo ya wilaya ya Kilwa katika kutekeleza sera ya kuyainua makundi hayo kwa kipindi cha 2018\2019 imeyapatia mikopo hiyo yenye masarti nafuu.

Mwenge wa Uhuru leo umehitimisha mbio zake katika halmashauri na wilaya ya Kilwa na kukabidhiwa katika manispaa ya Lindi. Ambapo kesho unatarajiwa kuhitimisha mbio zake kwa kuzimwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli katika uwanja wa Ilulu uliopo katika manispaa hii ya Lindi.

No comments:

Post a Comment

Adbox