Adbox

Sunday, October 13, 2019

Uniti 10 za damu salama zakusanywa kwenye mkesha wa Mwenge wa Uhuru Kilwa

Na Ahmad Mmow, Lindi.

Jumla ya uniti kumi za damu salama zimekusanywa katika mkesha wa Mwenge wa Uhuru katika viwanja vya bustani ya Mkapa( Mkapa garden) halmashauri ya mamlaka ya mji mdogo wa Kilwa Masoko.

Hayo yameelezwa leo na mkuu wa wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai wakati anakabidhi Mwenge wa Uhuru kwa halmashauri ya manispaa ya Lindi, mtaa wa Mtomkavu.

Ngubiagai alisema katika mkesha huo kulikuwa na uchangiaji damu salama,  wananchi waliojitokeza kuchangia walifanikiwa kutoa uniti kumi za damu salama.

Mbali ya damu salama, lakini pia mkuu huyo wa wilaya ya Kilwa alisema watu 47 walijitokeza kupimwa ili kuona kama wanavimelea vya ugonjwa wa malaria. Katika zoezi hilo ni watu wanne tu waliobainika kuwa na vimelea vya ugonjwa huo.

Lakini pia watu 247 walijitokeza kupima maambukizi  ya Virusi Vya UKIMWI( VVU). Katika upimaji huo wa maambukizi ya VVU ni mtu mmoja tu alikutwa na maambukizi,'' alisema Ngubiagai.

 Katika halmashauri ya wilaya ya Kilwa, Mwenge ulitembelea, kufungua na kuzindua miradi mitano ya maendeleo yenye thamani ya shilingi 1,900,000,000.

No comments:

Post a Comment

Adbox