Adbox

Thursday, October 24, 2019

Messi aweka Rekodi mpya michuano ya UEFA

Baada ya kufunga goli jana kwenye mechi dhidi ya Slavia, Messi amekua mchezaji wa kwanza kufunga goli kwenye misimu 15 ya Champions League mfululizo.

Maana yake ni kwamba tangu msimu wa 2005/2006 hadi leo 2019/20 Messi bado anacheka na nyavu kila msimu kwenye Champions League.

Msimu wa 2011/12 ndio alifunga magoli mengi ambayo ni 14, huku jumla hadi sasa amefunga jumla ya magoli 113 kwenye Champions League pekee.

No comments:

Post a Comment

Adbox