Adbox

Thursday, October 24, 2019

Serikali yamsaka aliyetangaza ujio feki wa Dreamliner nchini

Serikali kupitia Waziri ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano nchini Tanzania, imeagiza anayeendesha mtandao wa ATCL Aviation TV kukamatwa kwa kutangaza kuwa ndege nyingine mpya aina ya Dreamliner inakuja nchini wakati si kweli.

"Nimeagiza atafutwe nimemwambia na Waziri wa Mambo ya Ndani (Kangi Lugola) kuangalia sheria ya kumshtaki. Kama hakuna sheria tutamsumbua tu mpaka wenzake wamuonee huruma," amesema Kamwelwe.

Waziri Kamwelwe ameeleza hayo leo jijini Dar es Salaam katika kongamano la Tehama lililowakutanisha wadau mbalimbali wa sekta hiyo kujadili mchango wake kwa maendeleo ya uchumi wa viwanda.

Amesema kila jambo lina mamlaka zake za kutangaza na kama ni suala la ndege, wizara yake ndio ina dhamana ya kutangaza.

Amesema ameliuliza Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) wakamueleza kuwa hawakifahamu chombo hicho, nao pia wanashangaa.

No comments:

Post a Comment

Adbox