Adbox

Thursday, October 24, 2019

Mmiliki wa mtandao wa Facebook awekwa kitimoto

Mmiliki wa mtandao wa Facebook, Mark Zuckerberg amefika mbele ya Kamati ya Huduma za Fedha ya Baraza la Wawakilishi nchini Marekani kujibu maswali kuhusu mradi wake wa sarafu ya kidijitali inayofahamika kama Libra.

Zuckerberg alikabiliwa na maswali mengi kuhusu uingiliaji wa uchaguzi, uhuru wa kujieleza, makundi ya kueneza chuki na habari bandia, kutoka kwa wabunge.

Ushahidi wake umekuja siku mbili tu baada ya kampuni hiyo kufichua kuondolewa kwa mtandao akaunti za Urusi zinazowalenga wapiga kura wa Marekani kwenye jukwaa lake la Instagram.

No comments:

Post a Comment

Adbox