Na. Timothy Itembe Mara
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Saimon Sirro amekemea baadhi ya wanaume wanaowatesa wake zao na kuwakata masikio kwa mapanga huku wakiachwa wakiwa na vilema vya kudumu.
Sirro alisema hayo jana kwenye mkutano wa hadhara wakati akizungumza na watu wa Nyamongo kuhusu masuala ya ulinzi na usalama.
Sillo alisema kuwa ukatili kwa wanawake na watoto hauna budi kukomeshwa kwani vitendo hivyo havikubaliki katika jamii hususani kizazi hiki cha Sayansi na tekenolojia.
Kwa upande wake mkuu wa Jeshi la polisi mkoa wa kipoliis Tarime na Rorya,Henry Mwaibambe alisema kuwa katika mkoa wake wa kipolisi kuna ukatili mwingi juu ya wanawake na watoto ikiwemo ukeketaji kwa watoto wa kike.
"Ukatili wa kijinsia,watoto kubakwa na kupewa mimba mashuleni pamoja na wanawake kupigwa na wanaume na wengine kukatwa masikio kwa mapanga vimekidhiri kwa Tarime mfano kwa mwaka jana 2018 matukio yalikuwa 30 huku mwaka huu kuna tukio moja tu la ukatili lililoripotiwa"alisema Mwaibambe.
Mwaibambe aliongeza kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha kuwa ukatili kwa wanawake na watoto wa kike unamalizika na wanafanyashuguli za kimaendeleo kwa uhuru.
Naye Diwani viti maalumu kata ya Matongo, Filomena Tontora alisema kuwa matukio ya ukatili wanaofanyiwa wanawake hapo Nyamongo yamekidhiri hususani vipigo kwa wanawake wa nyumbani na wale wanaofanya kazi ya kuuza baa wanateswa sana ikiwemo kubakwa na kupewa mimba mashuleni.
Diwani huyo aliomba Jeshi la polisi kutofumbia macho ukatili wa kijinsia kwani wanaokuwa watenda ukatili huo wanafahamika na wakikamatwa wanarudi mitaani kutamba.
Tontora alimaliza kwa kupongeza Rais John Pombe Magufuli baada ziara yake wilayani Tarime iliyozaa matunda na kukomesha mauaji kwa wanyamongo waliokuwa wakiuawa ndani ya mgodi pasipo sababu ya msingi.
Wednesday, October 30, 2019
IGP Sirro asikitishwa na vitendo vya ukatili wa Kijinsia, atoa tamko
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment