Adbox

Monday, October 28, 2019

Askofu Msaidizi awasimika Mashemasi wapya,awataka wakamtumikie Mungu

Na. John Walter-Babati-Manyara

Askofu Msaidizi  wa Jimbo kuu katoliki la Arusha Mhashamu Prosper Lymo amewataka Mashemasi wannne waliopata daraja hilo takatifu kutumia vipawa walivyo navyo katika kujitolea kumtumikia mungu.

Wito huo ameutoa katika Misa takatifu ya kuwapatia daraja ya ushemasi mashemasi hao, iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Yosefu Parokia ya Magugu jimbo katoliki la Mbulu.

Mhashamu Baba Askofu amewasisitiza watii wito huo kwa kuwahubiria  watu Injili kama alivyokuwa akiifundisha Bwana Yesu Kristu.

Misa hiyo Takatifu imehudhuriwa na waamini,viongozi wa kanisa Katoliki wakiwemo watawa wa mashirika mbalimbali ,mapadre wa jimbo la Mbulu,pamoja na mapandre na masista wa shirika la wa palotini kutoka jimbo katoliki la Singida.

Mashemasi hao wa shirika la wapalotini ni George Kimina,Faustini Fransis,Gonzaga Mtaawe,na Mikaeli Muhia.

Ushemasi ni mashuhuda wa utakatifu wa watu wa Mungu unaopata chimbuko lake katika maisha ya Sala za Kanisa, Tafakari ya Neno la Mungu na Nidhamu katika maisha ya Utii, Useja na Ufukara kama kielelezo makini cha ufuasi wa Kristo kwa njia ya maisha ya wakfu.

No comments:

Post a Comment

Adbox