Adbox

Friday, October 25, 2019

Asakwa na Polisi kwa kumkata mkewe sikio

Mkazi wa Kijiji cha Mesaga Wilayani Serengeti Mara, aitwaye Magori anadaiwa kumkata masikio yote mawili Mke wake Mkami Mwitonyi mwenye umri wa miaka 22 kwa madai ya kupoteza simu yake, Mwanamke huyo amelazwa Hospitali ya DDH wodi ya Wanawake tangu October 23,2019 kwa matibabu zaidi.

Akisimulia tukio hilo Kaka wa Mwanamke huyo Muhoni Mbusi amedai ulitokea ugomvi kati ya wanandoa hao kisha Magori akachukua kamba na kumning'iniza Mkewe juu ya dari na kumkata sikio la kwanza na la pili huku akimwambia sali sala yako ya mwisho nakuchinja, wakati anajiandaa kumchinja Mwanamke akapiga kelele kwa nguvu majirani wakawahi kutoa msaada.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara Juma Ndaki amethibitisa na kusema wanaendelea kumtafuta mtuhumiwa ili afikishwe kwenye vyombo vya sheria.

No comments:

Post a Comment

Adbox