Na. Ahmad Mmow, Lindi
Diwani wa Kata ya Songosongo wilayani Kilwa, Said Mgeni amewaomba Waziri wa Uvuvi, Luhaga Mpina na Naibu wake, Abdallah Ulega kwenda Songosongo wakati wa ufunguaji miamba darasa.
Mgeni alitoa wito huo wakati wa ufunguaji mwamba darasa uliofanyika katika eneo la kisiwa kidogo cha Konjove kijijini Songosongo.
Alisema rasilimali zilizopo katika eneo hilo na kata ya Songosongo siyo mali ya kata wala kijiji hicho, bali taifa. Kwahiyo mawaziri au naibu wanaposhindwa kwenda kuonana na wananchi nikuwakatisha tamaa.
Mgeni ambae muda mwingi katika mazungumzo yake alilimwagia sifa na pongezi shirika la kuhifadhi mazingira duniani(WWF), kwa kutoa elimu, kuwezesha vikundi vya ulinzi shirikishi wa rasmali za baharini (BMU) na kufadhili shughuli zinazohusu utunzaji na usimamizi wa mazingira, alisema kwenda kushuhudia yaliyofanyika na changamoto zilizopo kutachochea na kuzidisha ari ya wananchi kulinda raslimali zilizopo baharini. Kwani watatumia nafasi hiyo kuzungumza na wananchi wa hapo ambao kazi yao kubwa ni uvuvi.
''Wasiishie Kilwa Kivinje, waje wakutane na wananchi wawahamasishe ili wasikate tamaa kulinda. Hapa tunapata shida hata fedha kupata kupitia BMU zinakwisha kugharamia ulinzi.
Wavuvi ambao vijiji vyao havifungi miamba wanatusumbua sana, kwahiyo wakija watapata nafasi ya kuwatia moyo wananchi wa hapa,''alisema Mgeni.
Mgeni ambae katika ufunguaji huo alifanikiwa kuvua pweza wenye uzito wa takribani kilo kumi alitoa wito kwa maofisa uvuvi waendelee kuvihamasisha vijiji ambavyo havina utaratibu wakufunga miamba vianze kufunga miamba yake ili kuwapunguzia majukumu wananchi wa kata yake , ikiwamo la ulinzi wa raslimali za baharini.
Alisema iwapo vijiji vyote vitafunga miamba itakuwa nirahisi kuwadhibiti wavuvi haramu. Kwani wananchi wa vijiji hivyo watashiri jukumu la ulinzi badala ya jukumu hilo kuachwa kwa BMU peke yake.
Monday, September 30, 2019
Waziri Mpina na Naibu wake wapewa mwaliko huu
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment