Rais wa shirikisho la soka nchini Uganda Moses Magogo ametangaza kujiweka pembeni kwa kipindi cha miezi miwili ili kupisha uchunguzi na nafasi yake ikakalimiwa na makamu wa Rais wa kwanza wa FUFA.
Kiongozi huyo anakabiliwa na tuhuma za kuuza kinyume na taratibu tiketi 177 za Kombe la Dunia mwaka 2014 tofauti na ilivyoelekezwa na FIFA
Kwa kawaida FIFA hutoa tiketi za fainali za Kombe la Dunia kila zinapofanyika katika mashirikisho ya soka wanachama, kwa lengo la shirikisho husika kuwauzia raia wa nchini kwake ambao watapenda kwenda kuangalia fainali hizo ila Magogo anatuhumiwa kuuza tiketi hizo nje ya Uganda.
Allan Ssewanyana ambaye pia ni mwandishi wa habari za michezo ndio alipelekea tuhuma hizo zilizopelekea Moses Magogo kutangaza kujiweka pembeni kwa kipindi cha miezi miwili.
Monday, September 30, 2019
Rais wa FUFA atangaza kujiweka pembeni kwa miezi miwili
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment