Adbox

Monday, September 30, 2019

BREAKING: Watuhumiwa 467 waomba kukiri makosa ya uhujumu uchum, Rais Magufuli aongeza siku

Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP), Biswalo Mganga amesema ofisi yake imepokea barua za watuhumiwa 467 wanaoomba kukiri makosa ya uhujumu uchumi na wapo tayari kurudisha fedha jumla ya Sh107.8 bilioni.

DPP ameyasema hayo leo wakati akipokea taarifa ya utekelezaji wa Ushauri alioutoa wa kuwasamehe Watuhumiwa wa Uhujumu Uchumi walio tayari kutubu na kurejesha Fedha na Mali.

Hata hivyo, Biswalo Mganga  amemuaomba Rais John Magufuli kuongeza siku tatu kwaajili ya kuwapa nafasi watuhumiwa wa uhujumu uchumi walio tayari kutubu na kurejesha fedha na mali.

Hata hivyo Rais Magufuli ameongeza siku saba kuanzia leo Jumatatu Septemba 30, 2019  kwaajili ya kuwapa nafasi watuhumiwa wa uhujumu uchumi walio tayari kumuandikia barua DPP ya kuomba kutubu na kurejesha fedha na mali.

No comments:

Post a Comment

Adbox