Adbox

Monday, September 23, 2019

Wawili wafariki Dunia ajali ya ndege Serengeti

Rubani na abiria mmoja wamefariki dunia baada ya ndege ndogo ya Kampuni ya Auric Air kuanguka leo asubuhi katika uwanja mdogo wa ndege Seronera, Serengeti. Taarifa ya Tanapa inasema abiria wote ni raia wa Tanzania.

Hata hivyo hadi sasa chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika.

Kamishna Msaidizi Mwandamizi Mawasiliano wa TANAPA,Pascal Shelutete amethibitisha na kusema ndege hiyo ilikuwa na Watu wawili pekee na wote wamefariki na kwamba taarifa zaidi ya kilichosababisha kutokea kwa ajali itatolewa na Mamlaka zinazohusika.

No comments:

Post a Comment

Adbox