Mkuu wa Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani, Asumpta Mshama amesema jiji la Dar es Salaam limejaa hivyo ukaribu na jiji hilo sanjari na uwepo wa barabara na njia nyingine za usafiri kunatoa fursa kwa Kibaha kupaa kiuchumi.
"Kwa hiyo tunazo fursa nzuri sana, ni vizuri mtu kabla hujafikiria kwenda kokote uwaze Kibaha, na sasa hivi tunajenga mji mpya hapa, watu waliokuwa wanawekeza badala ya kulala Dar es Salaam watakuwa wanalala hapa kwa hiyo tupo vizuri, ukitaka mahali pazuri pa kuwekeza hasa viwanda Kibaha tupo vizuri alisema ofisini kwake mjini Kibaha.
Ameyasema hayo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Maonesho ya Viwanda Mkoa wa Pwani 2019 na Kongamano la Fursa za Biashara na Uwekezaji mkoani humo.
"Kwanza Dar es Salaam kumejaa sasa watu wanatoka Dar es Salaam. Na kingine tuseme Tanzania nzima kama utasafiri kupita chini lazima upite Kibaha kuondoa tu Lindi na Mtwara. Lakini ukitoka Moshi, Arusha, Bukoba, wapi Kigoma kuondoa hiyo mikoa mingine lazima utapita Kibaha," amesema Mshama.
Amesema ofisini kwake kuwa, wilaya hiyo inajengwa kwa kuzingatia mpango uliopo na kwamba, kuna maeneo rasmi yaliyotengwa kwa ajili ya viwanda.
"Yamepimwa, wewe ukiomba huna zaidi ya mwezi una hati unaendelea. Urasimu sasa umepungua," amesema na kuongeza kuwa suala lalugha pia limezingatiwa.
Monday, September 23, 2019
Jiji la Dar limejaa - DC Kibaha
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment