Adbox

Monday, September 23, 2019

Patrice Evra atuma ujumbe Man United kufuatia kichapo kutoka kwa West Ham United

Kufuatia kipigo dhidi ya West Ham United, aliyekuwa nahodha wa Man United, Patrice Evra ametuma ujumbe wa wazi kwa Bodi ya Manchester United kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Ikumbukwe Man United bado haijateua mkurugenzi wa ufundi, inaonekana Evra ameweka jina lake kwenye nafasi hiyo.

"Nadhani ni wakati wa mikono yetu kuwa michafu, Bodi ya Manchester United mko tayari kuturuhusu tuwasaidie...?" ameeleza Evra.

Wakogwe wenzake Rio Ferdinand na Dimitar Berbatov wamekuwa wakihusishwa kupewa kazi hiyo ambayo bado iko wazi toka itangazwe miezi sita iliyopita.

No comments:

Post a Comment

Adbox