Naibu Waziri wa Kilimo, Omari Mgumba amewataka walimu wa shule za Msingi na Sekondari waache kutumia kilimo kama adhabu ya kuwapa wanafunzi wakati wanapokosea kwani inawajengea tafsiri mbaya kwa jamii na baadae wanapokuwa wanachukia kilimo.
Mgumba alisema hayo wakati wa ziara yake wilayani Pangani ambapo alisema kwamba kuna tabia ambayo imejengeka kwa walimu hao kwamba mtoto anapokosea anaambiwa leo utakwenda kilima siku nzima, utakwenda kumwagilia hali ambayo inapelekea baadae wakikua wanakuwa hawahitaji kilimo kwa sababu awali waliona kama adhabu.
Alisema kwamba hapana suala hilo sio jema na ndio maana wao wanasema kilimo ni ute wa mgongo lakini watafungamanisha kilimo na elimu ili watoto tokea anakuwa ajue kwamba nchi hii uchumi wake unategemea kilimo.
“Hivyo ninapoambiwa niwe na tuta la mchicha sio adhabu bali ni sehemu ya kuniandaa kielimu nije kujitegemea au nije kuajiri wengine kwenye mashamba yao kwani bila kufanya hivyo tutakuwa tunaimba kitu kingine wakati uchumi wetu unategemea kilimo”Alisema Naibu Waziri huyo.
Naibu Waziri huyo alisema kwamba mkakati wa serikali ni kuimarisha kilimo hivyo wataendelea kufungamanisha elimu yao na kilimo chao.
Akizungumzia Kilimo cha Minazi wilayani humo Naibu Waziri huyo alisema kwamba kilimo cha minazi ni kweli mpaka sasa hawaapata ufumbuzi wa magonjwa yake kwa miaka zaidi ya 30 mpaka leo ambayo yanasababsihwa na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Alisema pia hilo linatokana na kukubali kuletewe mbegu ya kisasa ambayo haiendani na mazingira ya nchi hivyo kama Taifa wameendelea kuimarisha vituo vyao vya utafiti hasa cha utafiti wa minazi mikocheni lengo ni kuanza kurudi kwenye kuzalisha miche kutumia minazi ya asili inayokabiliana na hali ya hewa na ikolojia ya ya nchi yetu.
“Na sasa tumeanza kuzalisha kitalu cha miche asili Bagamoyo na itasambazwa nchi nzima kwa lengo la kupanda na hatimaye kuweza kurejesha minazi hiyo”Alisema.
Akizungumzia udogo wa bei ya nazi nchini Naibu Waziri huyo alisema kwamba nazi zinauzwa bei ndogo na imeendelea kuwa ndogo ni kutokana na ushindani uliopo kwenye soko la ndani, kanda na kimataifa kwa sababu ya bidhaa mbadala.
“Hivyo kila nazi ikipanda bei watu wanakwenda kutumia mafuta lakini kila tunapoacha kutumia nazi na kutumia mafuta na kwenda kwenye chukuchuku wanapunguza mahitaji ya nazi”Alisema.
Hata hivyo alisema kwamba wanakuja na mkakati wa kuanzisha viwanda ambavyo vitaongeza thamani bidhaa hiyo ili kupanua soko la nazi hapa nchini na mbegu za nazi ambazo zinaweza kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi huku akieleza kwamba wakienda kuongeza thamai tatizo hilo litakwisha.
Monday, September 30, 2019
Walimu watakiwa kuacha kutumia Kilimo kama adhabu kwa wanafunzi
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment