Na Ahmad Mmow, Lindi
Wananchi wa kijiji cha Songosongo katika wilaya ya Kilwa wamelipongeza na kulishukuru shirika la kimataifa la uhifadhi na utunzaji mazingira duniani(WWF) kwa uvumilivu uliosababisha waanze kufaidi matunda ya uvumilivu huo.
Jana wakizungumza kwenye ufunguzi wa mwamba darasa, uliofanyika katika bahari ya Hindi katika kijiji hicho, walisema shirika hilo lilikutana na vikwazo vingi wakati linaanza kutoa elimu kwa wananchi wa kijiji hicho ambao kazi kubwa inayowaingizia kipato ni uvuvi.
Said Mgeni, ambaye ni diwani wa kata ya Songosongo alisema WWF lilipata upinzani kutoka kwa wananchi wakati linaanza kutoa elimu kuhusu uhifadhi na usimamizi wa mazingira. Ikiwemo madhara ya uvuvi haramu na faida za uvuvi salama.
Alisema wananchi walipandikizwa dhana mbaya kwamba WWF iilitaka kujimilikisha maeneo. 4: Diwani huyo alisema vikwazo hivyo havikulikatisha tamaa shirika hilo,bali liliendelea kutoa elimu ambayo wananchi wameanza kunufaika nayo.
''Kwetu sisi, WWF nikama baba wamafanikio yanayoonekana sasa. Leo huwezi kueleweka ukimuambia mtu wa Songosongo mwamba usifungwe ili avue muda wote kama zamani. Wameona faida ya kupumzisha mwamba,'' alisema Mgeni.
Mmvuvi Zainab Hassan alisema elimu hiyo imesaidia kuongeza uzalishaji wa samaki. Hasa aina ya Pweza.
''Leo ndani ya saa moja tu nimepata kilo ishirini za pweza. Kabla ya kupata elimu kutoka kwa WWF tulikuwa hatupati. Waliokuwa wanapata niwenye uwezo mkubwa tu, tena wazamiaji wenye uwezo wa kwenda mbali na hapa,'' alisema Zainabu. Alitoa wito kwa serikali ivihimize vijiji vingine vilinde na kufunga miamba yake.
Monday, September 30, 2019
Kijiji cha Songosongo waishukuru na kuipongeza WWF
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment