Adbox

Friday, September 6, 2019

RC Mara aipa kazi TALGWU

Na. Timothy Itembe Mara 

Mkuu wa mkoa Mara, Adamu Kigoma Malima amesema Chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa TALGWU kina nafasi kubwa ya kukemea na kutoa taarifa za matukio ya ukatili wa kijinsia badala ya kujikita katika kutetea masilahi ya wafanyakazi tu.

Malima alisema hayo jana kwenye kikao cha miaka miwili na Nusu tangu wakutane mwaka julai 2016 kilichofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Tarime jana cha kutimiza matakwa ya kikatiba ya chama.

Malima alisema kuwa Chama cha Wafanyakazi wa serikali za mitaa TALGWU kinasimamia wafanyakazi katika kutetea masilahi yao lakini pia kuna haja Chama hicho kuenda mbali zaidi kwa lengo la kukemea ukatili wa kijinsia ndani na nje ya watumishi kwa ujumla

Akitolea mfano wa mwalimu ambaye hakumutaja jina lake wala shule ya Msingi anayofundisha alisema kuwa hivi karibuni  Mwalimu moja wa shule ya msingi  alimbaka mwanafunzi wake  wa darasa la saba chumabani kwake huku akiwa amemfungia ndani huku  nje ya mlango akiwa amefunga  nakufuli.

“Niwatake Chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa TALGWU badala ya kujikita katika kutetea masilahi ya watumishi na mogogoro ndani ya wafanyakazi tu jaribu kwenda mbali zaidi ili mkatetee na kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto  unaofanywa na baadhi ya watumishi kwa tamaa zao na kufanya hivyo mtakuwa mnasaidia kazi serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli kwani jamani nasema uongo hayo hayafanyiki humu ndani au hakuna ukatili wa kingono kwa wafanyakazi?”alisema Malima.

Pia alikitaka Chama hicho kukemea ukatili wa kingono kwa baadhi ya watumkishi wa kike unaofanywa na baadhi ya mabosi wao pindi wanapokuwa wamefika kutafuta msaada na suluhu ya matatizo yanayowakabili.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa TALGWU mkoa Mara,Karebu Kehongo alimpongeza Rais awamu ya Tano John Pombe Magufuli kwa kushugulikiana kutatua baadhi ya  changamoto zinazowakabili wafanyakazi.

Kehongo alitumia nafasi hiyo kumuomba mkuu wa mkoa Mara kutatua changamoto zinazowakabili ikiwemo kutolipwa fedha za kujikimu kwa waajiriwa wapya wa kada ambazo sio walimu,mfano watendaji wa kata,vijiji na mitaa walioajiriwa kuanzia mwaka 2017 hadi sasa kwa baadhi ya halmashauri hawajalipwa.

Kutolipwa malipo ya likizo na matibabu kwa watumishi wasio waalimu,kutolipwa fedha za wastaafu kurudishwa nyumbani kulikosababisha waajiri wengi kupelekwa mahakamani,kutolipwa madai mengine kama uhamisho mapunjo ya mishahara hasa kwa watumishi waliokuwa wameondolewa katika utumishi wa umma na kurejeshwa japo maelekezo ni warejeshwe na kulipwa mishahara yao yote.

Naye katibu wa Chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa TALGWU mkoa Mara,Mussa Mashamba alisema kuwa ndani ya mkoa wake kuna kesi Saba za madai zinazohusisha  madai ya watumishi wastaafu kutorejeshwa Nyumbani kwao.

No comments:

Post a Comment

Adbox