Adbox

Friday, September 6, 2019

Afisa Utumishi Tarime ashinda nafasi ya kiti cha Kamati ya utendaji Taifa TALGWU

Na Timothy Itembe Mara

Afisa Utumishi na Utawala wa Halmashauri ya Tarime Vijijini, Kelven Mkirya amewabwaga wapinzani wake na kujinyakulia kura zote za ndio 139 kwenye nafasi ya uwakilishi wa  kiti cha kamati ya utendaji Taifa iliyokuwa  wazi ikigombewa ndani ya Chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa TALGWU.

Mwenyekiti wa Chama hicho mkoa Mara,Karebu Kehongo aliwaambia wajumbe ambao walihudhuria  na wapiga kura  kuwa kuna haja ya kuchagua mtu mahiri na makini na sio kuchagua kwa kufuata mahusiano ya  mtu bali wanataka kiongozi mchapa kazi.

Kehongo alitaja nafasi zingine zilizokuwa zinagombewa kuwa ni pamoja na kamati tendaji mkoa,Bunda halmashauri ya wilaya pamoja na halmashauri ya Mji wa Bunda,zingine ni kamati ya ushauri wafanyakazi wanawake mkoa,Musoma halmashauri na Musoma manispaa.

“Katika mkutano huu tutakuwa na mambo makuu matatu moja ni kutimiza matakwa ya kikatiba ya Chama ambayo inatutaka kufanya mikutano mikuu miwili ya mkoa kwa mda wa miaka mitano hivyo mkutano huu wa kipindi cha miaka miwili na nusu ,pili ni kufanya uchaguzi mdogo wa kuziba nafasi za uongozi wa mkoa na Kitaifa zilizosababishwa na sababu mbalimbali ikiwemo ya kustaafu,kufariki,kuacha kazi au kuachishwa kazi na tatu kutoa mafunzo kwa viongozi wote wa matawi na ngazi ya mkoa”alisema Kehongo.

Kwa upande wake mgeni rasimi ambaye ni mkuu wa mkoa Mara, Adamu Malima alitumia nafasi hiyo kuwataka wajumbe ili  kuchagua   kiongozi Bora wa kuwatumikia wanachama  na kutatua changamoto zinazowakabili badala ya kuchagua viongozi kwa kutazama  sura ya Mtu.

 Malima alionyesha  sura yake  kukerwa na vitendo vya ukatili wa kijinsia wanawake na watoto kwenye jamii  ambapo alitumia nafasi hiyo kukemea vitendo  hivyo  ndani ya jamii na ndani ya watumishi baadhi yao wakiomba rushwa ya ngono watumishi ndipo watatue shida zao huku wakijua kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.

Malima aliwataka wajumbe wa mkutano wa Chama cha wafanya kazi wa serikali za mitaa TALGWU  kutoa taarifa sehemu husika pindi wanapoona vitendo hivyo vikifanyika ndani ya maeneo yao ili hatua zichukuliwa.

No comments:

Post a Comment

Adbox