Adbox

Friday, September 6, 2019

Rais Magufuli amuomba Rais Yoweri Museven kubadilisha uongozi wa URA

Rais John Magufuli amemuomba Rais wa Uganda Yoweri Museven kubadilisha uongozi wa Mamlaka ya Kodi Uganda (URA), kwa kuchelewesha mradi wa bomba la mafuta kutoka Hoima hadi Tanga kutokana na masuala ya kodi.

Amesema hayo leo kwenye ufunguzi wa kongamano la Biashara kati ya Tanzania Uganda ambalo limefanyika leo Dar es Salaam.

"Simfundishi kazi mzee Museveni lakini nilimwambia mimi wakati naingia madarakani nimefukuza makamishna general wa TRA watano na wewe yule wa kwako wa URA anakuchelewesha na anachelewesha maendeleo ya wagand," amesema.

Ameendelea kwa kusema "Nilimwambia wazi sitaki kuwa mnafki na nawaambia watendaji i wish watendaji wangu wangeenda Uganda na waUganda wangekuja huku nidili nao kidogo"- *Dokta John Pombe Magufuli.

No comments:

Post a Comment

Adbox