Adbox

Sunday, September 22, 2019

Rais wa Iran aitaka nchi yake kuongoza ulinzi wa eneo la Ghuba

Rais wa Iran Hassan Rouhani amesema leo nchi yake ndiyo inapaswa kuongoza juhudi za usalama kwenye eneo la Ghuba na kuwa iko tayari kushirikiana na mataifa mengine ya eneo hilo.

Akizungumza wakati wa gwaride la kijeshi mjini Tehran, Rouhani amesema nchi yake inanyoosha mkono wa kirafiki na kidugu kwa mataifa mengine ya kanda hiyo katika kusimamia ulinzi wa eneo la Ghuba na ujia muhimu wa Hormuz, unaopitisha kiasi asilimia 20 ya mafuta ghafi duniani.

Rouhani amesema uwepo wa vikosi vya jeshi kutoka mataifa ya kigeni katika eneo la Ghuba unaweza kusababisha matatizo kwa usalama wa nishati ulimwenguni.

Matamshi ya Rouhani yanakuja wakati Marekani inatuma vikosi zaidi vya kijeshi nchini Saudi Arabia kuimarisha ulinzi kwa washirika wake wa Kiarabu.

Marekani inaituhumu Iran kuwa nyuma ya mfululizo wa mashambulizi kwenye miundombinu ya mafuta yaliyotokea karibuni nchini Saudi Arabia, madai ambayo Tehran inakanusha.

No comments:

Post a Comment

Adbox