Adbox

Monday, September 23, 2019

Mtoto wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania afariki ajali ya ndege

Mtoto wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo, Nelson Mabeyo ni mmoja wapo kati ya watu wawili waliofariki katika ajali ya ndege ya Kampuni ya Auric iliyotokea leo asubuhi.

Nelson ndio  alikuwa rubani wa ndege hiyo iliyoanguka katika uwanja mdogo wa ndege wa Seronera uliopo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti nchini Tanzania.

Ndege hiyo ilianguka saa 1:30 asubuhi wakati ikipaa katika uwanja huo kwenda mkoani Arusha.

Habari za uhakika kutoka mamlaka ya viwanja wa ndege imeeleza kuwa Nelson aliondoka na ndege hiyo jana katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam.

Akizungumza katika uwanja wa ndege wa Soronera, Msimamizi wa Kampuni ya Auric, Peter Kimaro amesema Nelson amefariki katika ajali hiyo akiwa na Nelson Orutu ambaye ni rubani mwanafunzi.

No comments:

Post a Comment

Adbox