Wanafunzi saba wamethibishwa kufariki na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya darasa la shule yao kuporomoka mapema Jumatatu asubuhi jiji la Nairobi nchini Kenya.
Jengo la mbao la shule ya msingi ya Precious Talent liliporomoka muda mfupi kabla ya masomo ya siku kuanza. Wanafunzi 50 wamelazwa hospitali kwa ajili ya matibabu katika mji mkuu wa Nairobi, kulingana na msemaji wa serikali Cyrus Oguna.
Kituo cha televisheni nchini Kenya NTV kimetuma picha ya ujume wa Bwana Oguna kupitia Twitter akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la tukio ambapo jengo liliporomoka, akiwahakikishia wazazi kwamba serikali italipia garama ya matibabu ya wanafunzi waliojeruhiwa:
Monday, September 23, 2019
Wanafunzi 7 wafariki baada kuangukiwa na paa la darasa
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment