Rais wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli amewataka Maofisa Watendaji wa Kata kutembea kifua mbele kwa kuwa mwajiri wao ni Rais wa Jamhuri ya Tanzania, na wao ndio wawakilishi wake katika kata zao.
Kauli hiyo aliitoa Ikulu, Dar es Salaam, alipokuwa akizungumza na watendaji hao wa kata nchi nzima.
Alisema kuwa anajua wana majukumu mengi na wanakumbana na changamoto kutoka kwa wakubwa wao, wakiwemo makatibu tarafa na wakurugenzi wa halmashauri, lakini pia kwa nafasi yao wanaweza kuwawajibisha viongozi hao.
“Nimewaita hapa ili kuwapa meno, mtambue kuwa ninyi ni mabosi, asitokee yeyote wa kuwatisha, tembeeni kifua mbele. Nyie ndio mnaosimamia kata zenu, mna wajibu wa kuhakikisha maelekezo ya Serikali yanatekelezwa kikamilifu kwa ajili ya kuwezesha uelewa kwa wananchi.
“Akitokea kiongozi yeyote niliyemteua anamnyanyasa kiongozi wa kata, nitamuona hatoshi, na nitasikitika zaidi akitokea kiongozi yeyote wa kata akimnyanyasa mwananchi wangu aliyekaa juani akanipigia kura, naye nitamuona hatoshi,” alisema.
Tuesday, September 3, 2019
Mtambue kuwa ninyi ni Mabosi, asitokee wa kuwatisha - Rais Magufuli
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment