Ofisa Uhamasishaji wa klabu ya soka ya Yanga, Antonio Nugaz amefunguka kuwa wao ni wakimataifa licha ya kupoteza mchezo wa klabu bingwa Afrika dhidi ya Zesco.
Pia Nugaz amewashukuru mashabiki wote ambao wameisupport timu yao maana imetoka upande wa kulia na imeingia kushoto.
"Kwa sasa sisi ni wa kimataifa, kushindwa kwetu kutinga hatua ya makundi haina maana ya mwisho wa mbio kimataifa bali tunaingia kwenye kombe la shirikisho huko tutapambana," amesema Nugaz.
"Shukrani kwa mashabiki kwa sapoti kubwa na Yanga tumeonyesha maana ya kuwa wa kimataifa tumetoka kulia tumeingia upande wa kushoto," amesema," ameongeza.
Yanga ilitolewa na Zesco kwenye michuano ya klabu bingwa kwa jumla ya mabao 3-2 na kutupwa mpaka kwenye michuano ya kombe la Sshirikisho.
Sunday, September 29, 2019
Antonio Nugaz awatuliza mashabiki wa Yanga na kichapo cha Zesco
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment