Watu Tisa wanaodaiwa kujihusisha na matukio ya utapeli kwa kutumia simu za mkononi na laini za simu kutoka makampuni mbalimbali na orodha ya namba za simu za watu wamekamatwa na Jeshi la Polisi Mkoani Pwani.
Watu hao walikuwa wakituma ujumbe mfupi sms kwamba watumiwe pesa na kujifanya waganga wa jadi na wanazindika, kusafisha nyota za watu, ndoa na biashara.
Akithibitisha kuhusiana na tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani, Wankyo Nyigesa alieleza, Agosti 13 mwaka huu, Kata ya Zinga na Yombo wilayani Bagamoyo walikamatwa watuhumiwa hao wakiwa na simu za mkononi 14, laini za simu za makampuni mbalimbali 22 na orodha ya namba ya simu za watu 16 zilizoorodheshwa kwenye karatasi.
Aliwataja majina yao kuwa ni, Suleimani Athuman (35), Hamis Iddi (30), Dipinde Pango,Adam Nestory, Hamis Kondo, Deus Swai , Julius Joseph(27) na Mohammed Bruno (33).
Wankyo alibainisha kuwa watuhumiwa hao wanahojiwa ni namna gani wanafanya uhalifu wao kwa kutumia mtandao ya simu na kufanya wizi wa pesa kwa kuchepusha salio la pesa ya mtu kwa makusudi ya uhalifu.
“Watafikishwa mahakamani baada ya mahojiano na uchunguzi kukamilika”alifafanua Kamanda huyo.
Wednesday, August 14, 2019
Watu Tisa wakamatwa kwa utapeli wa kutumia Simu
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment