Gazeti la kila wiki la The East African ililoingia katika usambazaji Agosti 10, 2019 limenukuliwa likiarifu umma kuwa watumishi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wamejiondoa katika vituo vyao vya kazi kutokana na kutolipwa mishahara.
Habari hiyo inatia doa katika haiba ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Wana Jumuiya na pia kwa wadau wa maendeleo.
Katika taarifa ya Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhandisi Steven Mlote, amefafanua kuwa taarifa zilizochapwa na gazeti hilo sio za ukweli. Aidha, ameeleza kuwa mishahara ya watumishi ya mwezi Julai ishalipwa.
"Kuthibitisha taarifa hizo, tuliwasiliana na Mwenyekiti wa Wabunge wa Afrika Mashariki kutoka Tanzania Mheshimiwa Dkt Abdullah Hasnu Makame ambaye alithibitisha kuwa hali ni shwari na hapana taharuki. Watumishi wamelipwa mishahara yao na majukumu ya kila siku yanaendelea kutekelezwa," ameeleza.
Aliongeza kuwa Dkt Makame alihimiza umuhimu wa nchi wanachama kuwasilisha michango yao kwa wakati, kwani kwa kufanya hivyo wataiwezesha Jumuiya kutekeleza majukumu yaliyopangwa na Wanachama wake kwa weledi na ufanisi mkubwa.
Wednesday, August 14, 2019
Jumuiya ya Afrika Mashariki yavunja ukimya kuhusu kuyumba kiuchumi
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment