Wachezaji 48 wa timu ya mpira wa miguu kutoka nchini Tanzania wamekabidhiwa bendera ya Afrika Mashariki tayari kuelekea katika Mashindano ya Ligi Ndogo East Afrika yatakayofanyika jijini Nairobi nchini Kenya.
Wakizungumza katika Makao makuu ya Afrika Mashariki Nahodha wa wachezaji hao Lukumay Ally amesema kuwa wanatarajia kupata ushindi mnono na kuiletea taifa heshima katika michuano hiyo ya kimataifa.
Mkurugenzi wa Upendo Friends school ambaye ni mmiliki wa Upendo Friends academy Isabella Mwampamba amesema kuwa michuano hiyo itaisaidia Tanzania kushiriki mechi za kimatifa na kuibua vipaji muhimu ambavyo vitakua lulu kwa taifa.
Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika Masuala ya Mipango na Miundombinu Steven Mlote amesema kuwa michezohiyo ni chachu katika kukuza na kuendeleza mtangamano wa Afrika Mashariki.
Wednesday, August 14, 2019
Wachezaji 48 kuiwakilisha Tanzania michuano ya Ligi ndogo East Afrika CUP
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment