Rais Magufuli ametengua uteuzi wa DED wa Halmashauri ya Morogoro Vijijini, Kayombe Rioba kwa utendaji usioridhisha wa miradi ya maendeleo hususani ujenzi wa Hospitali ya Wilaya.
Uamuzi wa kuondolewa kwa kiongozi huyo umetangwa na Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Seleman Jafo leo.
"Leo tarehe moja mwezi wa 8 mwaka 2019, Mh. Rais Magufuli amemtengua Mkurugenzi wa Halashauri ya Wilaya ya Morogoro Bwn. Kayombe Masoud Rioba kutokana na usimamizi usioridhisha wa miradi ya maendeleo hususani ujenzi wa Hospitali ya Wilaya," amesema leo Waziri Jafo.
No comments:
Post a Comment