Adbox

Tuesday, July 23, 2019

Vimelea vya malaria vyaota sugu dhidi ya dawa

Kuna sababu ya Afrika kuhofia usugu wa vimelea wa malaria dhidi ya dawa?

Uchunguzi wa vimelea vya vinasaba (DNA) ulionyesha usugu ulisambaa kote Cambodia kama ilivyokuwa katika maeneo ya Laos, Thailand na Vietnam.Haki miliki ya pichamapigo.com
Image captionUchunguzi wa vimelea vya vinasaba (DNA) ulionyesha usugu ulisambaa kote Cambodia kama ilivyokuwa katika maeneo ya Laos, Thailand na Vietnam.
Usugu wa vimelea vya ugonjwa wa malaria dhidi ya dawa muhimu unaonekana kusambaa haraka katika maeneo ya Kusini Mashariki mwa Asia wanasema watafiti kutoka Uingereza na Thailand.
Vimelea wamehama kutoka Cambodia hadi Laos, Thailand na Vietnam, ambako nusu ya wagonjwa hawaponi kwa dawa wanazochagua.
Watafiti wanasema kuwa matokeo ya utafiti yanaibua "hali ya kutisha kwa siku zijazo" kwamba usugu dhidi ya madawa unaweza kusambaa hadi Afrika . Hata hivyo wataalamu wanasema athari zake zinaweza kutokuwa mbaya kama ilivyofikiriwa. thought.

Ni nini kinachofanyika ?

Malaria hutibiwa kwa mchanganyiko wa dawa mbili ambazo ni - artemisinin na piperaquine.
Mchanganyiko huu ulianzishwa nchini Cambodia mwaka 2008.
Lakini kufikia mwaka 2013, visa vya kwanza vya mabadiliko ya kimelea na kujenga usugu kwa dawa zote viligundulika, katika maeneo ya magharibi mwa nchi hiyo.
Utafiti wa hivi karibuni uliochapishwa katika jarida la kitabibu la Lancet la magonjwa ya maambukizi, ulitathmini sampuli za damu kutoka kwa wagonjwa wa maeneo mbali mbali ya Kusini mashariki mwa Asia.
Uchunguzi wa vimelea vya vinasaba (DNA) ulionyesha usugu ulisambaa kote Cambodia kama ilivyokuwa katika maeneo ya Laos, Thailand na Vietnam.
Pia ulionyesha kuwa vimelea vilibadilika zaidi, na kuvifanya kuwa hata tatizo zaidi.
Katika baadhi ya kanda, 80% ya vimelea wa malaria vilikuwa sugu kwa dawa.
"Usugu huu umeenea na kusambaana umekuwa mbaya zaidi ," Dkt Roberto Amato, kutoka tasisi ya Wellcome Sanger , aliiamba BBC.

Je hii inamaanisha kuwa ugonjwa huu unaelekea katika hali ya kutotibika ?

Hapana.
Utafiti mwingine, uliochapishwa na jarida hilo hilo la Lancet , ulionyesha kwua nusu ya wagonjwahawakuweza kutibiwa na kiwango cha kawaida.
Hata hivyo, kuna dawa nyingine mbadala ambazo zinaweza kutumika.
" Huku kukiwa na hali ya kusambaa na kuimarika kwa usugu wa vimelea, matokeo ya utafiti wetu yanaonyesha dharura inayohitajika kutumia matibabu mbadala ya awali ", Amesema Profesa Tran Tinh Hien, Mtafiti wa masuala ya Tiba katika Chuo Kikuu cha Oxford alipokuwa Vietnam.
Hii inaweza kujumuisha matumizi ya dawa tofauti sambamba artemisinin au kutumia mkusanyiko wa dawa tatu ili kukaliana na usugu wa vimelea.

Hofu ni ipi?

Mafanikio makubwa yamefikiwa katika kuutokomeza ugonjwa wa malaria.
Hata hivyo kujitokeza kwa kwa usugu wa dawa kunatishia mafanikio ya kuutokomeza.
Suala jingine ni kama usugu wa vimelea vya malaria utaeneo katika maeneo ya mbali zaidi na kufika barani Afrika, ambako kuna watu tisa kati ya wanaugua ugonjwa huo.
" Vimelea hawa wa Malaria waliofanikiwa kuwa na usugu dhdi ya madawa wana uwezo wa kuvamia maeneo mengine mapya na kupata jeni mpya na hivyo kusababisha hofu kwa siku zijazo kwamba wanaweza kusambaa hadi Afrika ambako visa vya malaria viliwahi kujenga usugu miaka ya 1980 , na kusababisha vifo vya mamilioni ya watu," amesema Profesa Olivo Miotto, kutoka taasisi ya Wellcome Sanger na Chuo Kikuu cha Oxford.

Hii inaleta mabadiliko gani kwa watu wanaoishi katika maeneo huko?

Matokeo ya uchunguzi hayatabadili mengi katika kaisha ya kila siku ya katika jimbo la Greater Mekong Subregion, Kusini Mashariki mwa Asia.
Kukabiliana na malaria ni zaidi ya kupata tu tiba sahihi baada ya kupata ugopnjwa.
Juhudi zote kuanzia udhibiti wa kusambaa kwa mbu wanaoeneza ugonjwa haitaleta mabadiliko.
Hata hivyo , watafiti wanasema dawa ambazo watu wanapewa baada ya kupata ugonjwa zinapaswa kubadilika.
Tafiti pia zinaonyesha kuwa utafiti wa Jeni za vimelea vya malaria unaweza kuwasaidia madaktari kuwa hatua moja mbele ya usugu wa vimelea vya malaria unaojitokeza ili kuwapatia wagonjwa tiba sahihi.

Je hii ni picha halisi?

Kuenea kwa usugu ni habari mbaya dhidi ya kushuka kwa visa vya malaria katika kanda hiyo ya Kusini Mashariki mwa Asia.
"Vimelea hawa wanatisha, bila shaka," Prof Colin Sutherland, kutoka taasisi ya dawa za maeneo ya joto mjini London, amesema.
"Hata hivyo, Niajiuliza kama vimelea hawa hawako katika hali nzuri sana kwasababu kwa ujumla idadi yao inaangamia."

Nchini Cambodia kulikuwa na:

  • Visa 262,000 vya malaria mwaka 2008
  • Visa 36,900 vya malaria mwaka 2018
Kwa hiyo, huku bila shaka usugu wa madawa wa vimelea umesambaa, sio lazima kuwa ni tisho la dunia, kwamujibu wa Profesa Sutherland.
"Athari sio mbaya sanakama tunavyoweza kufikiria," amesema.

Malaria ni mbaya kwa kiasi gani?

Kuna visa takriban milioni 219 vya malaria kote duniani kila mwaka.
Dalili za ugonjwa huo ni pmaoja na kusikia baridi mwilini, na kutetemeka ambako hufuatiwa na kupanda kwa joto mwilini na kutokwa na jasho jingi.
Bila matibabu, vimelea wanaweza kumsababishia mgonjwa matatizo ya kupumuana kuharibika kwa viungo vya ndani vya mwili.
Malaria huwauwa watu wapatao 435,000 kila mwaka-wengi wao wakiwa ni watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.

Uneweza pia kutazama:

Mbwa kutambua ugonjwa wa Malaria kwa kunusa

No comments:

Post a Comment

Adbox