Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewatoa hofu wananchi kutokana na kuwepo
kero ya upatikanai wa vitambulisho vya taifa, alisema hakuna mwananchi atakayekosa kitambulisho hicho na mwanzoni mwa
Wiki hii amewaelekeza Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), kutoa namba kwa wakati ili waweze kufanyiwa na usajili wa simu zao za mkononi.
“Narudia tena, kitambulisho ni haki ya kila mwananchi na hakuna atakayekosa kitambulisho cha taifa, pia nimewaelekeza NIDA waniletee takwimu za Wilaya zote ili kujua ukubwa wa tatizo la
usajili wa vitambulisho hivyo unavyoendelea,” alisema Lugola.
Pia, Waziri Lugola alisema Tanzania ina amani kwasababu inautamaduni wa kuwa na amani, hivyo asitokee mtu akaharibu utamaduni huo ambao nchi inaendelea kuhudumisha.
“Ndugu zangu wana Mwiseni, Wana Mwibara, amani tulionayo ndiyo inatuwezesha leo tunalima vizuri, tunavua samaki, leo tunakula vizuri, leo tunafanya shughuli mbalimbali za maendeleo,
hivyo tuendelee kuitunza amani hii,” alisema Lugola.
Aliongeza kuwa, Wizara yake kupitia Jeshi la Polisi ipo imara, Serikali ya Rais Dkt. John Magufuli ipo imara na inaendelea kuwalinda Watanzania mahali popote walipo nchini, na hakuna mtu atakaye ivunja amani hiyo
No comments:
Post a Comment