Adbox

Friday, July 5, 2019

Makanisa, Misikiti itakayokwepa kuhakikiwa kuchukuliwa hatua kali - Waziri Lugola



Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amesema Makanisa na Misikiti nchini ambayo itashindwa kwenda kufanyiwa uhakiki itachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

Waziri Lugola ameyazungumza hayo katika Mkutano wa hadhara wa Wananchi wa Kijiji cha Mwiseni, Kata ya Butimba, Jimbo la Mwibara, Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara, leo, ambapo alifafanua kuwa; uhakiki huo ni lazima na unalenga kuzifuatilia taasisi hizo za dini kujua utendaji wake wa kazi kama unaendana na sheria za usajili.

Lugola amesema Serikali haikuweza kuendelea na usajili wa Makanisa na Misikiti pamoja na Taasisi za kiroho nchini, wakati kwa hivyo ikaona ifanye uhakiki kwanza kwa lengo la kujua taasisi hizo zinaweza sawa na sheria za usajili.

“Tuhakikishe tunaendesha Makanisa na Misikiti na hizi taasisi za kiroho na kijamii kwa mujibu wa masharti ambayo mmesajiliwa kufanya, na pale ambapo utakuta, Kanisa lolote, Msikiti wowote,
taasisi ya kiroho yoyote inafanya shughuli zake kinyume na kusajiliwa kwake, kujihusisha na mambo ambayo hawaruhusiwi, sisi kama Wizara tumeapa kumsaidia Mhe. Rais tutachukua hatua kwa mujibu wa sheria na utaratibu,” alisema Lugola.

No comments:

Post a Comment

Adbox