Rais wa Marekani akizungumza kuhusu Uturuki kununua mfumo wa kujihami na makombora wa S-400 kutoka nchini Urusi amejibu swali kuhusu mfumo huo kwa kusema kwamba Marekani haina haja kuiadhibu Uturuki kwa kununua mfumo huo.
Akiwa ikulu White House, Donald Trump amehoji kana kwamba mataifa wanachama wa jeshi la kujihami la Magharibi NATO yameanza kuwekeana vikwazo baina yao akimaanisha kuwa Uturuki ni mwanachama wa NATO ambalo linaashiria kuwa hakuna vikwazo vya aina yeyote dhidi ya Uturuki kwa kununua mfumo huo wa kujihami na makombora kutoka nchini Urusi.
Rais wa Uturuki aliwahi kuzungumza kuhusu suala hilo kabla ya kuondoka kujielekeza nchini Japan mwezi ulipita kushiriki katika mkutano wa G-20.


No comments:
Post a Comment