Ofisi za Baraza Kuu la Waislamu (BAKWATA)Katika Wilaya Mpya ya Kigamboni zimezinduliwa Rasmi. Hafla hiyo iliyotanguliwa na Ghafla ya uzinduzi wa usambazaji wa Katiba ya Bakwata Toleo la 2019, Katiba hiyo ilizinduliwa na Samahal Mufti wa TanzaniaSheikh Abubakar Bin Zubeir mwaka huu.
Mgeni Rasmi katika ghafla ya uzinduzi wa Usambazaji Katiba hiyo ya BAKWATA alikuwa Mhe Dkt Abdullah Hasnu Makame - Mwenyekiti wa Wabunge wa Afrika Mashariki kutoka Tanzania.
Samahal Mufti aliiagiza Jumuiya ya Vijana ya Bakwata (JUVIKIBA) ifanye usambazaji wa Katiba hiyo nchini ambapo iliamuliwa zoezi hilo lianzie Kigamboni.
Mwenyeji wa ghafla hizo pacha alikuwa Sheikh Abdullah Iddi Alhadhramy - Sheikh wa Wilaya ya Kigamboni.
Hadhara hiyo ilihudhuriwa na Mheshimiwa Dotto Msiwa, Diwani wa Kigamboni pamoja na Masheikh na Vijana kutoka Bakwata katika ngazi za Taifa, Mkoa, Wilaya hadi kata.
Monday, July 15, 2019
Ofisi ya BAKWATA wilayani Kigamboni yazinduliwa
Tags
# Habari
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Habari
Tags:
Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment