Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI, Mwita Waitara,ameagiza kila mtumishi wa umma kote nchini kuhakikisha anasimamia miradi ya serikali iliyopo katika maeneo yao.
Waziri ametoa agizo hilo mkoani Njombe wakati akizungumza na baadhi ya watumishi wa umma katika kikao cha tathmini ya elimu cha halmashauri ya wilaya ya Njombe kilichofanyika mjini Njombe.
“Hakuna kukumbatia mradi kama ni wa kwako lazima tushirikiane miradi ya maendeleo ikamilike na fedha ambazo zimeletwa ziende kwenye miradi iliyokusudiwa,kinyume na hapo utakutana na mkono wa sheria,unaenda kwenye miradi unakuta mkurugenzi peke ake ndio anayejua wenzake wamejitoa hawashiriki,unaende kwenye elimu anayejua ni afisa elimu wengine hawapo,huo utaratibu ni marufuku”amesema Waitara
Aidha waziri huyo amepiga marufuku kwa mtumishi yeyote wa serikali kujihusisha na maswala ya kisiasa.
“Ukisha kuwa kiongozi mfano mkuu wa shule majukumu yako ni zaidi ya mtumishi wa kawaida,hata maneno yako inabidi ubadirike kwasababu kuna watu wanakufuatilia,yako maneno sana huko ambayo yanatengenezwa na wanasiasa halafu wapo watumishi wanayabeba,mimi nikukute unamsema rais mtaani ili hali ni mtumishi wa serikali halafu unaisema serikali sasa ukipatikana huyo anayekutuma hawezi kukusaidia,wewe ni sehemu ya serikali”aliongeza Waitara
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth msafiri amesema halmashauri tatu zilizopo katika wilaya yake zimeendelea kushirikiana katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo huku halmashauri hizo zikifanikiwa kukusanya zaidi ya asilimia mia moja ya makisio yao kwa mwaka wa fedha uliopita.
“katika mwaka wa fedha uliokwisha halmashauri zote tatu ziliweza kukusanya zaidi ya asilimia mia moja ya makisio yao,hii maana yake ni kwamba kwa usimamizi na maelekezo ambayo tumepewa wanasimamia vizuri katika miradi ya wananchi”amesema Ruth msafiri
No comments:
Post a Comment