Dirisha la uhamisho linakaribi lakini bado kuna uhamisho mkubwa unaotarajiwa kufanyika.
Kwa baadhi imekuwa kama kizungumkuti. Atakwenda? au Atasalia? Ni maswali yatakayojibiwa kadri muda unavyosogea na kuwadia kufungwa kwa dirisha la uhamisho kwa klabu za England 17:00 BST siku ya Alhamisi Agosti 8.
- Mo Salah atua Nairobi
- Pacquiao amchokoza Mayweather
- Bondia afariki baada ya kuumizwa vibaya ulingoni
Haya ndio baadhi ya masuala makuu ambayo yangali kutatuliwa...
Bale ataishia wapi?
Atakwenda wapi? Atagharimu fedha kiasi gani? Ni kwanini Real Madrid ina hamu ya kumuondoa?
Haya ndio maswali ambayo yatabaini mustakabali wa Bale, mchezaji huyo wa kimataifa wa Wales huko Uhispania wakati muda unayoyoma wa dirisha la uhamisho kuwa wazi.
Winga huyo wa Real Madrid aliyesajiliwa kwa rekodi wakati huo ya kitita cha £85m alipotoka Tottenham Septemba 2013. Ameshinda katika La Liga na mataji manne ya ubingwa Ulaya.
Mkufunzi wa Real Zinedine Zidane wiki hii amesema Bale ana "anakaribia kuhamia klabu nyengine " na kufichua kuwa mchezaji huyo alikataa kucheza kama mchezaji wa akiba katika mechi ya Jumapili ya kabla ya kuanza msimu dhidi ya Bayern Munich huko Houston. Bale alicheza na kufunga katika mechi ya urafiki dhidi ya Arsenal lakini Zidane ameongeza kuwa, licha ya kushiriki mechi hiyo, 'hakuna kilichobadilika'.
Kwa mujibu wa ripoti, klabu ya katika ligi kuu ya Uchina Beijing Guoan inataka kumsajili Bale na Paris St-Germain imejadiliana kuhusu uwezekano wa kufanya mageuzi na mchezaji wa kiungo cha mbele wa Brazil Neymar. Inadhaniwa kwamba hamu ya Manchester United kumsajili imepoa.
Lukaku anaelekea Italia?
Mshambuliaji wa Manchester United Romelu Lukaku amehusishwa pakubwa na uhamisho kwenda Inter Milan msimu mzima wa joto lakini makubaliano yaliofikiwa....mpaka sasa.
Pendekezo la £53.9m la Inter lilikataliwa na United Jumamosi muda mfupi baada ya klabu hizo mbili kukabiliana katika mechi ya kabla ya kuanza msimu.
Aliyekuwa mkufunzi wa Chelsea, Antonio Conte tayari alikuwa amekiri kuwa Lukaku ni mchezaji 'anayependa' na kusisitiza baada ya kushindwa katika mechi ya Jumamosi kwamba anahisi Lukaku anaweza "kukiimarisha kikosi".
Mchezaji huyo wa miaka 26 alikosa mechi zote za utalii za United nchini Australia kutokana na majeraha kabla ya kukosa mechi ya Jumamosi huko Singapore.
United alimsajili Lukaku kwa pauni £75m kutoka Everton miaka miwili iliyopita na kuhisi kuwa pendekezo la Inter lipo chini ya thamani waliomuekea mchambuliaji huyo.
Mmoja ndani, mmoja nje ya Spurs?
Mchezaji mwingine aliyegonga vichwa vya habari msimu huu w ajoto ni beki wa Tottenham Danny Rose.
Mchezaji huyo wa miaka 28 alikiri mnamo Juni kwamba hana hakika ya mustakabali wake na aliruhusiwa kusalia England kutafuta kalbu zitakazovutiwa naye wakati timu ya kwanza ilipoelekea katika ziara Asia.
Juventus imehusishwa kutaka kumsajili Rose, wakatia taarifa nyingine zikiashiria kuwa Tottenham itamuwania mlinzi wa Fulham Ryan Sessegnon iwapo beki huyo wa kushoto ataondoka.
- Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 24.07.2019
- Ronaldo aponea shtaka la 'ubakaji'
- Makocha waliotimuliwa baada ya Afcon 2019
Sessegnon, ambaye anapokea matibabu kwa sasa ya jeraha la msuli wa hamstring amesalia na mwaka mmoja katika mkataba wake huko Craven Cottage.
Liverpool, Paris St-Germain, Juventus na Borussia Dortmund zote zimehusishwa na kumsajili mchezaji hyo chipukizi wa miaka 19.
Je Palace itaendelea kumzuia Zaha?
Winga wa Crystal Palace, Wilfried Zaha amesema anataka kuondoka katika klabu hiyo msimu huu wa joto na kupendelea uhamisho kwenda Arsenal.
Mchezaji huyo wa kimatiafa wa Ivory Coast ataacha pengo kubwa huko Palace, ambayo tayari imempoteza beki mahiri Aaron Wan-Bissaka kwa thamani ya £50m kwenda Manchester United.
Arsenal imewasilisha ombi la ufunguzi la thamani ya £40m mapema mwezi huu lakini Palace inavutiwana maombi ya thamani inayokaribia £80m kwa Zaha, aliyesaini mkataba mpya msimu uliopita wa joto . Tangu hapo bosi wa rsenal Unai emery amsema klabu hiyoingali inajaribu kusajili, "wachezaji wakubwana wenye gharama".
Hatahivyo huenda wakakabiliwa na uhindani. Ripoti za hivi karibuni zinaashiria Bayern Munich imeibuka na kuwashangaza wengi baada ya kushindwa kumsajili Leroy Sane wa Manchester City na Bale wa Real Madrid.
Maguire anahama?
Mlinzi wa Leicester Harry Maguireamehusishwa kwenda Manchester United kwa msimu mzima wa joto, lakini Leicester, haina nia ya kumuuza.
United ilijitoa kwenye mazungumzo mwak ajana baada ya kuhisi thamani aliyowekewa mchezaji huyo wa miaka 26 ilipita kiasi lakini ilirudi kuwasilisha ombi jingine kwa thamani kama hiyo mapema mwezi huu.
Mlinzi huyo wa timu ya taifa ya England ameleeza hamu yake kutaka kucheza katika kiwango cha juu lakini Leicester inaamini ana thamani zaidi ya £70m, huku meneja Brendan Rodgers akisema tthamani yao haijafikiwa.
Baadhi ya taarifa sasa zinaashiria mkataba wa £80m umefikiwa lakini je Maguire atajiunga na United kabla ya msimu wa joto na je kuna nfasi nyingine zozote?
Majina mengine makuu yanayotajwa?
Kuna na suala dogo la Paul Pogba.
Mchezaji huyo wa kiungo cha kati wa Manchester United ameng'ang'ana kufikia kiwango alichokuweko katika klabu ya Juventus na amehusishwa na uhamisho nje ya England msimu huu.
Kumekuwa na uvumi kwamba mustakabali wa Pogba huko Old Trafford baada ya kutaja "changamoto mpya" mnamo Juni, wakati ajenti wake amesema raia huyo wa Ufaransa anataka kuondoka.
Mnamo Julai, meneja wa United Ole Gunnar Solskjaer amesema Pogba hajawahi "kuwa tatizo" na kudai kuna "ajenda" didi ya mchezaji huyo.
Wakati huo huo, mahasimu wa mji Manchester City inatarajia winga wa Ujerumani Sane atasalia katika klabu hiyo licha ya hamu ya Bayern kutaka kumsajili .
Guardiola amesema waajiri wake wa zamani wamekuwa wakijadili kuhusu azma yao kwa muda mrefu lakini amewaambia waandishi habari wiki iliyopita hakuzungumzana yoyote kutoka klabu hiyo ya Ujerumani kuhusu uwezekano wa kufikiwa makubaliano.
Kwengineko mchezaji wa kiungo cha kati wa Arsenal Mesut Ozil hatojiunga na klabu ya Uturuki Fenerbahce, baada ya klabu hiyo kusema haiwezekani kwa mtazamo wa kiuchumi kumsajili mchezaji huyo.
Mwezi Januari Emery amesema "hafikirii" kuhusu Ozil kuondoka, lakini anataka mchezaji huyo awe na msimamo.
No comments:
Post a Comment