Vikosi vya uingiliaji kati wa haraka katika maeneo yenye ghasia (RSF) vimekuwa vikishutumia kufanya maasi kote nchini Sudan yakiwemo mauaji ya kikatili ya mwezi Juni ambapo watu 120 waliripotiwa kuuawa, huku wengi miongoni mwa waliouawa wakitupwa katika mto Nile. Mtaalam wa masuala ya Sudan Alex de Waal amezungumzi kuhusu umaarufu kikosi hiki.
RSF kwa sasa ndio wanaoitawala Sudan. Kwa sasa wao ni aina mpya ya utawala: Aina ya wanamgambo wa kijamii na kampuni ya wafanyabiashara, kikosi cha mamluki wanaovuka mipaka ambao wameteka nchi.
Kamanda wao Jenerali Mohamed Hamdan "Hemeti" Dagolo, na wapijganani wake wametoka mbali tangu zamani walipokuwa wakiitwa wanamgambo wa kiarabu ambao baadae walitambulika mama "Janjaweed".
- Uingereza yaionya Iran baada ya kuiteka meli yenye bendera yake
- Ni kwanini chui alipatikana kitandani?
- Je unaweza kuamini FaceApp yenye sura yako?
- Picha bora za Afrika : Siku za mvua na mawimbi makubwa
Kikosi hiki cha uingiliaji kati wa haraka -RSF awali kilianzishwa kutokana na mamlaka aliyokuwa nayo aliyekuwa rais-President Omar al-Bashir mwaka 2013. Lakini wanamgambo wa kikosi hicho 5,000 tayari walikuwa wana wanamiliki silaha hata kabla.
Hadithi yao ilianza mwaka 2003, wakati serikali ya Bwana Bashir ilipowaachisha kazi wapiganaji wafugaji wa kiarabu Arab herders to fight ili kukabiliana na wapiganaji wa waafrika katika jimbo la Darfur.
' Janjaweed ni akina nani'
Janjaweed walikuwa ni wafugaji wa ngamia wanaohama hama kutoka tawi la Mahamid na Mahariya kutoka kundi la jamii ya Rizeigat wa kaskazini mwa jimbo la Darfur na maeneo ya Chad - Waliishi katika maeneo ya kando kando mwa jangwa hata kabla ya ramani za maeneo na nchi kuchorwa.
Wakati wa vita na mauaji ya Darfur ya kati ya mwaka 2003-2005 kiongozi wa kundi la Janjaweed alikuwa ni Musa Hilal, Chifu wa Mahamid.
Wakati wapiganaji hawa walipodhihirisha ufanisi wa kumwaga damu, Bwana Bashir aliwahalarisha rasmi na kuwafany akuwa kikosi cha kijeshi na wakaitwa Kitengo cha ujasusi wa mpakani (Border Intelligence Units).
Kipindi muhimu cha kazi ya Hemeti kilikuwa ni mwaka 2007, wakati vikosi vyake vilipokasirishwa na kushindwa kwa serikali kuvilipa mshahara.
Walihisi kuwa wanatumiwa vibaya, kuwekwa katika mstari wa mbele kwenye mapambano , kulaumiwa kwa maafa yanayotokea -halafu wanatelekezwa.
Ingawa makamanda wa Hemeti wote wanatoka katika ukoo wa Mahariya, alikuwa tayari kuwajumuisha watu kutoka makundi yote ya kikabila . Katika tukio la hivi karibuni kabisa RSF waliingizwa katika vuguvugu lililojitenga la waasi wa Sudan Liberation Army (SLA) - wanaoongozwa na Mohamedein Ismail "Orgajor", anayetoka katika kabila la Zaghawa - ambao pia wanatoka katika jimbo la Darfur ambao wamekuwa wakihusishwa na na waasi.
Kujumuisha mamlaka
Hemeti alirudi Khartoum alipopewa mkataba mtamu: malipo tena kwa vikosi vyake,vyeo kw amaafisa wake (akawa Brigadia Jenerali ),na malipo mazuri ya pesa.
Vikosi vyake viliwekwa chini ya usimamizi wa kitengo cha Ujasusi na huduma za usalama wa taifa (NISS), wakati wa maandalizi ya vita na Chad.
Baadhi ya wapiganaji wa Hemeti, waliokuwa wakihudumu chini ya upinzani wa Chadian walipigana hadi katika mji mkuu Chad , N'Djamena, mnamo mwaka 2008.
Wakati huo huo, Hemeti alikosana na mkubwa wake , Hilal - na hasira yao ndiyo iliyosababisha vita vya kwa miaka 10. Hilal alifahamika sana kwa ukataji wa viungo vya binadamu, na majenerali wa bwan Bashir wakaona Hemeti ndiye wa kutegemewa zaidi.
Mwaka 2013, kikosi kingine cha kijeshi kiliundwa chini ya Hemeti na kikaitwa RSF.
Mkuu wa majeshi ahakulipenda hilo - alitaka pesa ziende kuimarisha vikosi vya kawaida - na Bashiri alikuwa na hofu kubwa juu ya kuwapatia NISS mamlaka zaidi na akaamua tu kumfuta kazi mkurugenzi wa kikosi hicho kwa madai ya kufanya njama dhidi yake.
Kwa hiyo RSF waliwajibishwa kwa Bwana Bashir mwenyewe- rais akampa Hemetijina bandia la "Himayti", likimaanisha "mlinzi wangu".
Vikosi vya RSF vilipigana dhidi ya waasi katika jimbo la Kordofan Kusini - hawakuwa na nidhamu na hawakufanya kazi vizuri- tofauti na Darfur, ambako walifanya kazi vema.
Walikimbilia dhahabu.
Uhasama wa Hemeti na Hilal ulichacha wakati dhahabu ilipogundulika katika eneo la Jebel Amir katika jimbo la Darfur mnamo mwaka 2012.
Uhasama huu ulikuja muda mfupi tu wakati Sudan ilipokuwa ikikabiliwa na mzozo wa kiuchumi wakati Sudan Kusini ilipojitenga na kuchukua 75% ya utajiri wa mafuta, hii ilionekana kana kwamba ni kitu kiulichotumwa na Mungu.
Lakini ulikuw ani mkosi zaidi . Maelfu kwa maelfu ya vijana wadogo walikimbilia kwenye maeneo ya mbali ya Darfur kujaribu bahati yao ya kupata dhahabu kwa kutumia vifaa katili.
Baadhi walibahatika na kupata dhahabu na kuwa matajiri, wengine waliangukiwa na vifusi vya migodi na wengine waliuawa na sumu ya mercury inayotumiwa katika mchakato wa kufua dhahabu.
- Kuna matumaini ya kuwepo kwa Sudani mpya?
- Waziri Mkuu wa Ethiopia aingilia kati mgogoro wa Sudan
- Jeshi la Sudan lakemewa kwa kushambulia waandamanaji
Wanamgambo wa Hilal waliteka kwa nguvu eneo na kuwauwa watu zaidi ya 800 people kutoka kabila la Beni Hussein, na wakaanza kutajirika kw akuuza dhahabu.
Baadhi ya dhahabu zilizwa kwa serikali, ambayo ililipa zaidi ya bei ya sokoni kwa pesa ya Sudan kwasababu ilikuwa inataka sana kupata dhahabu ambayo ingeiuza nchini Dubai kwa pesa yenye thamani zaidi.
No comments:
Post a Comment